NONGA AREJEA MWADUI FC


Mchezaji Paulo Nonga amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kukubaliana na viongozi wa Mwadui na kwa pamoja kuamua kufanya biasha juu ya mchezaji huyo

Akiongea na Mwandike.blogsport,Nonga amesema kwamba amefurahishwa na maamuzi ya uongozi wa Yanga kwa kuweza kumruhusu kujiunga na Mwadui ambapo kabla ya kutua Y.anga alikua anaitumikia timu hiyo inayofundishwa na kocha Jamhuri Kiweru Julio

Amesema kwamba kutua ndani ya klabu hiyo kutamfanya apate nafasi kubwa ya kucheza kwani kunako klabu ya Yanga alikua hapati nafasi ya mara kwa mara baada ya kuzidiwa uwezo na wachezaji waliyopo kwenye nafasi anayocheza ikihusisha washambuliaji kama Dornad Ngoma na Amis Tambwe.


No comments