JKT RUVU WAUKUBALI KWA SHINGO UPANDE MKATABA WA AZAM MEDIA
Meneja wa timu ya JKT RUVU ya Kibaha mkoani Pwani,Duncan Beno
amesema kwamba udhamini wa Azam Media wa
bilioni 23 juu ya kupewa haki ya kuonyesha matangazo ya mpira wa miguu katika
michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara bado ni mdogo kutokana na gharama za
uendashaji ligi kua mkubwa
Akiongea na Saidaalymwandike.blogsport Beno amesema kwamba klabu zinatumia kiasi kikubwa cha fedha
kuweza kufanikisha kuendesha timu hivyo bado udhamini huo haukidhi matakwa ya
vilabu katika uendeshaji wa timu
Hata hivyo amedai kua maamuzi ya makubaliano ya mkataba huo kwa kiasi kikubwa wao hawakuhusika kwani liliopangwa na TFF ndilo lililopitishwa ingawa baadhi ya klabu hazikulizishwa na mkataba huo wa miaka mitano wenye thamani ya bilioni 23
Post a Comment