WANACHAMA WA YANGA WAKIONGOZWA NA JERY MURO WAENDA NYUMBANI KWA HAJI MANARA NA KUMKABIDHI MCHANGO WA FEDHA KWA AJILI YA MATIBABU


Baadhi ya mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga wakiongozwa na mkuu wa idara ya Habari wa klabu hiyo Jery Muro,usiku huu wameenda nyumbani kwa mkuu wa idara ya habari wa Simba Haji Manara na kufanikiwa kumkabidhi kiasi cha shilingi milioni moja na elfu hamsini kwa ajili ya kujikimu na matibabu


Haji Manara kwa sasa anasumbuliwa na macho ambapo toka wiki iliyopita jicho lake la kushoto halioni vizuri na  jicho la kulia nalo lina uoni hafifu na kwa sasa anatarajiwa kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi


Kwa mujibu wa taarifa kutoka baadhi ya mmoja wanachama wa klabu hiyo ya Yanga,amesema kwamba fedha hizo zimepatikana kwa kuchangishana kupitia makundi yao mbalimbali.


No comments