SIMBA KUWATAMBURISHA WACHEZAJI WAPYA SIKU YA TAMASHA LA SIMBA DAY


Baada ya kuonekana kwamba wachezaji mbalimbali kutoka nje ya nchi wanaendelea kufanya majalibio katika timu hiyo,uongozi wa timu ya soka ya Simba,umesema kwamba swala la wachezaji ambao watasajiliwa kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo litajulikana katika tamasha lao la Simba day ambapo uongozi utatumia fursa hiyo kuwatambulisha wachezaji wapya

Akiongea na Mwandike.blogsport,katibu mkuu wa klabu hiyo Patrick Kahemele amesema kwamba yote haya ambayo yanazungumzwa na baadhi ya watu juu ya usajili wa wachezaji wakiwemo kutoka nje ya nchi yatajulikana siku hiyo ya tamasha


Aidha amesema kwamba kwa sasa hawezi kulizungumzia swala zima la mchezaji Laudit Mavugo pamoja na Kipre Tchetche kwa kua kwa sasa hawana mpango wa kuzungumzia maswala hayo ya usajili ingawa kuna kumekua na taarifa zikihusishwa na wekundu hao kua mpango wa kutaka kufanya usajili wa wacjezaji hao wa kigeni


Kahemele amewataka mashabiki wa Simba kwa sasa wasiwe na wasiwasi juu ya usajili wa timu hiyo kwani viongozi wapo makini kwenye zoezi hilo na nia yao ni kuona msimu ujao wanakua na kikosi bora ambacho kitakua na chachu ya mafanikio makubwa

Timu ya Simba kwa sasa ipo kambini mkoani Morogoro ikiendelea kujiwinda na maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara chini ya kocha Josph Omog.

No comments