YANGA WAENDELEA KUGOMEA UDHAMINI WA AZAM MEDIA


Baada ya shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,kuweza kuingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya bilioni 23 na kampuni ya Azam Media juu ya haki ya kuonyesha mechi za ligi kuu ya Tanzania bara,leo hii uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba unataraji kukaa kwa ajili ya kulitolea ufafanuzi jambo hilo

Kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Baraka Deudetis amesema kwamba uongozi wa klabu hiyo unataraji kukaa kulitolea ufafanuzi jambo hilo lkn kimsingi amesema kwamba kwa upande wao haridhiki na mkataba huo

Amesema kwamba tangu awali Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji amejalibu kulizungumzia swala hilo ambalo kwa upande wao udhamini huo hauna faida kwao kwani unapunguza idadi ya mashabiki ambao wanaingia uwanjani na swala la mgawanyo sawa na timu nyingine ambazo hazina mashabiki ni jambo ambalo si kila ungwana.

No comments