AZAM TV YAINGIA MKATABA WA MIAKA 5 WENYE THAMANI YA BILIONI 23 KWA AJILI YA KURUSHA MECHI ZA LIGI KUU YA TZ BARA
Kampuni ya Azam Media imeingia mkataba wa kurusha
matangazo ya ligi kuu ya Tanzania bara wenye thamani ya bilioni 23 kwa kipindi
cha miaka mitano mara baada ya kufanikiwa kuyapiku makampuni mengine ambayo
nayo yalionyesha nia ya kutaka kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za ligi kuu
ya Tanzania bara
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii katika ofsi
za TFF,Mkurugenzi wa kampuni ya Azam Media Tiddo Muhando amesema kwamba kwa
upande wao wamefarijika kuwa washindi wa umiliki wa matangazo hayo kwani nia
yao ni kuona wanaleta chachu ya maendelea katika mpira wa miguu hapa nchini
Amesema kwamba mara baada ya kufanikiwa jambo hilo sasa
kilichopo ni kuhakikisha kua msimu ujao matangazo yao yanakua bora tofauti na
misimu mitatu ya nyuma
Nae mtendaji mkuu wa bodi ya ligi,Boniphace Wambura amesema kwamba mkataba huo ambao wenye thamani ya bilioni 23 kwa miaka mitano
ni tofauti na mkataba wa awali ambao huu wa sasa umekua na maboresho makubwa
ambayo yatazifanya vilabu shiriki kwenye michuano hiyo kuleta ushindani wa
kutosha
Amesema kwamba vilabu vingi vimekua havileti ushindani wa
kutosha kutokana na ukata wa fedha hivyo kwa mkataba huu anaamini kwa kiasi
kikubwa fedha hizo zitakua na manufaa kwa upande wao
Aidha amedai kua mgawanyo wa fedha hizo utagawanywa
katika awamu nne ambapo awamu ya kwanza hadi ya tatu kila klabu itapata milioni
42 huku awamu ya nne mara baada ya ligi kumalizika mgawanyo utakua mkubwa kwa
timu ambazo zimeshika nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi
Post a Comment