TFF WASEMA FEDHA ZA YANGA ZA UDHAMINI WA HAKI YA MATANGAZO YA TELEVISHENI ZIKO PALE PALE
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi,Boniphace Wambura amesema kwamba fedha za timu ya Yanga za udhamini wa haki ya matangazo ya televisheni kupitia kampuni ya Azam za msimu uliopita bado zipo na endapo klabu hiyo kama ina nia ya kuhitaji fedha hizo basi wanapaswa kwenda kuzichukua sehemu husika
Wambura ameyasema hayo hii leo wakati wa uingiaji mkataba mpya na kampuni ya Azam Media wenye haki ya kuonyesha mechi za ligi kuu ya Tanzania bara kwa miaka mitano mkataba wenye thamani ya bilioni 23 kwa fedha za kitanzania
Amedai kua haki ya kuonyesha mechi za ligi kuu ni mali ya TFF,hivyo hata kwa huu mkataba mpya kila timu itapata mgawo sawa katika awamu tatu ambapo kila awamu klabu itapata milioni 42 huku mgawo wa nne mgawanyo utazidi kwa kila timu ambayo imefanya vizuri katiaka ligi hiyo kwa kufuata msimamo.
Post a Comment