MCHEZO WA SERENGETI BOYS NA TIMU YA VIJANA YA KENYA WAOTA MBAWA


Mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Serengeti Boys na kikosi cha timu ya Taifa ya vijana cha Kenya sasa hautakuwepo baada ya timu ya Taifa ya Kenya kupata mwaliko wa kushiriki michuano ya COSAFA

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas ameiambia Saidallymwandike.blogsport kwamba wamepokea taarifa kutoka chama cha soka cha Kenya kuhusiana na taarifa hiyo ambapo amesema kwamba Kenya wamepata mwaliko wa michuano hiyo baada ya timu ya Taifa ya Msumbiji kujiondoa

Amesema kwamba licha ya kutokuwepo kwa pambano hilo lakini timu ya vijana ya Serengeti Boys itaendelea kujiandaa na mchezo wao wa kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana dhidi ya Afrika Kusini.

No comments