USAJILI WA WACHEZAJI WA MICHUANO YA AIRTEL RISING STAR KUANZA JUMATATU



Mashindano ya Airtel Rising Star yanataraji kuanza hivi karibuni ambapo leo imeandaliwa semina elekezi kwa ajili ya kupeana kanuni na taratibu mbalimbali kuelekea kwenye michuano hiyo ya vijana itakayojumuisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini

Akiongea na Mwandike.blogsport,Afsa habari na mawasiliano wa kampuni hiyo ya Airtel,Jane Matinde amesema kwamba dhamira yao ni kuendelea kuibua vipaji kwa vijana ambapo kupitia michuano mbalimbali iliyoandaliwa na kampuni hiyo imefanikiwa kuzalisha wachezaji wengi ambao wengi wao kwa sasa wamekua msada kwa timu za Taifa ikiwemo kikosi cha Serengeti Boys inayowania kusaka kucheza faianali za Afrika

Amesema kwamba zoezi zima la usajili kwa wachezaji linataraji kuanza siku ya jumatatu hivyo amewataka wadau wa michuano hiyo kuendelea kuinga mkono na wahusika wa timu wafanye usajili wa wachezaji ambao wana sifa za kushiriki michuano hiyo

Kwa upande wake katibu mkuu wa TFF,Mwesigwa Selestini ameishukuru kampuni hiyo kwa namna inavyojitoa kuwekekza katika soka la vijana ambalo ndilo chimbuka la wachezaji bora

Amesema kwamba maendeleo ya mpira wa miguu sikuo zote uanzia ngazi ya chini hata kwa wale ambao wamefanikiwa mara nyingi hua wanawekeza kwenye soka la vijana

No comments