NI BUKU 3,000 TU KUIONA MECHI YA YANGA NA MEDEAMA HAPO JUMAMOSI

Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzana bara timu ya soka ya Yanga umetangaza viingilio vya mchezo wao wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya timu ya Medeama ya Ghana ambapo kiingilio cha chini ni Sh 3,000 kwa sehemu zote na kwa majukwaa ya orange itakuwa Sh 5,000. Na Sh 15,000 kwa VIP A huku VIP B na C ni sh 10,000

Akiongea na Saidallymwandike.blogsport leo hii,Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deudetis amesema wameamua kuweka viingilio vya chini kabisa ili mashabiki wa klabu hiyo wapate nafasi ya kujitokeze kwa wingi katika pambano hilo linalotarajiwa kupigwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

Aidha amesema kwamba maandali kwa upande wa kikosi cha timu hiyo yanaendelea vizuri na kila mchezaji ana molari ya hali ya juu kuelekea kwenye pambano hilo.

No comments