YANGA YAENDELEA KUSUASUA KATIKA USHIRIKI WA MICHUANO YA KIMATAIFA


Matumaini ya timu ya Yanga kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika yameanza kupoteza kumwelekeo mara baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na timu ya Medeama kutoka nchini Ghana

Yanga ndio wamekua wa kwanza kupata bao kunako dk ya pili mfungaji akiwa Dornad Ngoma baada ya kumalizia pasi ya Thabani Kamusoko na kufanikiwa kuukwamisha mpira wavuni

Mara baada ya bao hilo Yanga ilionekana kudhamiria kupata bao lingine la pili lkn kukosa kwa umakini wa safu ya ushambuliaji kwa kutozitendea haki nafasi walizopata imewalazimu kushindwa kupata bao la kuongoza

Medeama ya nchini Ghana ilifanikiwa kutumia udhaifu wa Yanga kwenye nafasi ya kiuongo ambapo katika kipindi cha kwanza sehemu hiyo ikiongozwa na Thabani Kamusoko na Mbuyu Twite walishindwa kucheza kwa ufasaha

Benard Donso kunako dakika ya 17 alifanikiwa kuisawazishia bao Medeama kwa kuweza kufunga bao zuri kwa kisigino kufutia mpira wa kona uliopigwa na Enock Atta Adjel

Kipindi cha pili timu zote zilicheza kwa kushambuliana huku dk tano za mwanzo Medeama wakionekana kucheza kwa tahadhari kubwa na kutafuta nafasi ya bao lkn uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga ikiongozwa na Vicent Bossou na Calvin Yondan waliweza kuzuia mashambulizi

Mchezaji Amis Tambwe leo alishindwa kuitumia nafasi ya wazi ambae alibaki yeye na mlinda mlango lakini shuti lake  lilimlenga golikipa

Yanga walifanya mabadiliko katika kipindi cha pili kwa kumtoa,Osca Joshua,Amisi Tambwe na nafasi zao kuchukuliwa na Haruna Niyonzima na Juma Mahadhi lkn mabadiliko hayo hayakuweza kuisaidia Yanga kwani hadi mpira unamalizika timu hizo zimetoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1

Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kuburuza mkia kwenye kundi hilo wakiwa na alama moja wakicheceza mechi tatu huku wanaongoza kundi hilo ni TP Mazembe ambao wana alama sita baada ya kushuka dimbani mara mbili ambapo kesho watamenyana na Mo Bejaia ya Algeria

No comments