TFF YAITAKA YANGA KUACHA KUCHEZA KWA MAZOEZEA KATIKA MECHI ZA KIMATAIFA


Baada ya klabu ya Yanga kupigwa faini ya dola za kimarekani 10,000 ambazo zinakadiriwa kufikia shilingi milioni 22 za Tanzania kwa kosa la wachezaji wake kuchelewesha muda ili mchezo usiendelee wakati mwamuzi alipotoa adhabu ya penati kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Sagrada Esparenca ya Angola,hii leo shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limevitaka vilabu vya Tanzania ikiwemo Yanga kuacha mpira wa mazoea katika michuano ya kimataifa

Akiongea na Saidaallymwandike.blogsport,ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba ni vyema klabu za Tanzania zikaacha kucheza kwa mazoea kwenye michuano ya kimataifa kwani wakiendelea kufanya hivyo huenda wakakumbana na  adhabu kubwa kuliko hii ambayo wameipata Yanga ingawa klabu hiyo imetakiwa kulipa dola 5,000 baada ya dola 10,000 kwa sababu ni kosa la kwanza

Lucas amesema kwamba ni vyema vilabu vikatofautisha ligi ya hapa nyumbani na michuano ya kimataifa ksb ingawa ligi yetu ni bora lkn kuna tofauti kubwa ya kiutendaji kati ya michuano ya kimataifa na ligi za Tanzania

Hata hivyo kuelekea kwenye mchezo unaofuata wa kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Yanga na Medeema ya Ghana hapo jumamosi,shirikisho hilo limetoa tahadhari kwa viongozi wa Yanga kua makini na pambano hilo kwani wanaweza kukumbana na rungu la CAF endapo kutatokea mazingira ya utatanishi kama yale ambayo yametokea kwenye mechi dhidi ya TP Mazembe

No comments