BAADA YA KUSAMEHEWA KULIPA GHARAMA ZA UHARIBUFU WA UWANJA WA TAIFA,YANGA WAISHUKURU SERIKALI


Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Yanga,umeishukuru serikali kwa kuweza kuwasamehe kulipa gharama za uhalibufu wa baadhi ya maeneo katika uwanja wa Taifa baada ya kutokea vurugu kwenye mchezo wao wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Tp Mazembe ambapo mchezo huo mashabiki waliingia bure

Akiongea na Mwandike.blogsport,kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedit amesema kwamba jambo hilo ni faraja kwa serikali kutambua umuhimu wa Yanga kwenye ushiriki wa michuano ya kimataifa kwa kuzingatia kua ni timu pekee kwa ngazi ya klabu ambayo imesalia katika mashindano ya kimataifa

Amesema kwamba kutokana jambo hilo kwa viongozi wa klabu wamejipanga kuhakikisha hakutatokea uharibufu kama huo kwenye michezo yao ambayo watacheza uwanjani hapo kwa kuweza kuwaelimisha mashabiki wanaopata fursa ya kuingia uwanjani

No comments