MTIBWA SUGAR WAANZA MCHAKATO WA USAJILI WA WACHEZAJI

 
  
Baada ya kuondokewa na baadhi ya wachezaji nyota wa kikosi cha kwanza uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro,umesema kwamba kwa sasa wapo katika mchakato wa kufanya marekebisho mbalimbali katika kikosi cha timu hiyo kwa kuweza kufanya usajili ambao utakua na chachu ya kua na timu bora msimu ujao

Msemaji wa timu hiyo Tobiasi Kifaru amesema kwamba kwa sasa kikosi kimeshaanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara hivyo kwa sasa benchi la ufundi likiongozwa na kocha mkuu wa klabu hiyo Salum Mayanga ni kuhakikisha wanapata wachezaji bora wa kuziba mapengo yaliyopo

Aidha Kifaru ameshindwa kuweka bayana juu ya usajili unaofanywa na klabu hiyo ambapo kuna taarifa kua kwa sasa wamekamilisha usajili wa wachezaji wawili akiwemo Rashidi Mandawa aliyekua anaitumikia timu ya Mwadui pamoja na Cassian Ponera wa Ndanda ya mkoani Mtwara

Hata hivyo amesema kwamba uongozi wa klabu hiyo utaweka bayana majina ya wachezaji ambao watasajiliwa na klabu baada ya dirisha la usajili kufungwa kwani ndio itakua ndio wakati wa mwafaka kwa yeye kuyaweka hadharani majina ya wachezaji waliosajiliwa.

No comments