MASHINDANO YA UMITASHUMITA WILAYA YA ILALA YAANZA RASMI

Na,Mwandishi Wetu
Mashindano ya michezo kwa shule za msingi UMITASHUMITA  katika Manispaa ya Ilala leo yamezinduliwa rasmi ambapo michezo ya ainambalimbali itachezwa ili kupata wawakilishi wa Wilaya.

Akizungumza na  hadhara katika ufunguzi  wa michuano hiyo inayofanyika katika viwanja wa chuo cha Magereza Ukonga, Kaimu Kamishina wa Magereza Gideon Nkana , ameipongeza  timuzitakazoshiriki katika michuano hiyo ya kupata timu ya Wilaya itakayowakilusha katika mashindano hayo kwa ngazi ya Mkoa  na kuwataka wanamichezo kuwa na nidhamu na kujibidisha ili waweze kutetea Ubingwa wao.

Aidha alisema, Taifa bila  Michezo haliwezi kujipambanua  nakuharakisha maendeleo kielimu, kiuchumi, kijamii na Kiutamaduni hivyo pamoja na changamoto zilizopo michezo mashuleni hainabudi kuendelezwa na changamoto hizo ziweze chachu ya kuendeleza michezo.

"Hapa tunaondoka Kuna KLASTA nne nawaomba mchezo wa nidhamu ya hali ya juu hapa ndipo mnatakiwa muonyeshe vipaji vyenu michezo ni ajira hapa ndipo mnaweza kuendeleza vipaji vyenu na serikali itaendelea kuzifanyia kazi changamoto" . Alisema.

Alisema sekta ya Michezo inakabiliwa na changamoto ikiwemo ukosefu wa Viwanja  vya michezo na rasilimali fedha lakini Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuzungumza  na kuboresha  baadhi ya mambo.

"Napenda niwajushe kuwa nimekubali kuwa mlezi wenu na Nina ahidi kushirikiana na viongozi wenu na nitawapa ushirikiano wa kutosha." Alisema.
Kwa upande wake Afisa Elimu ya msingi wa Manispaa ya Ilala Elizabeth  Thomas, alisema mashindano hayo yameandaliwa katika hatua ya mchujo na wamegawa katika KLASTA nne katika wilaya ili kurahisisha  kuwapata washindi watakao wakilisha Wilaya katika mashindano ya Mkoa.

No comments