WANACHAMA WA SIMBA WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA MKUTANO MKUU

Uongozi wa klabu ya Simba umewataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi hapo kesho katika mkutano mkuu wa wanachama kwa ajili ya kujadili ajenda mbalimbali ambazo zitajadiliwa kwenye mkutano huo.

Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba,Haji Manara alisema kwamba mkutano huo utaanza saa nne asubuhi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere ukitanguliwa na wanachama kujiorodhesha majina yao.

Manara alisema kwamba anaamini mkutano huo utakuwa na tija kwa klabu kwani utajadili maswala mbalimbali ya klabu ikiwemo mapato na matumizi na kupitisha bajeti ya mwaka.

No comments