MRISHO KHALIFAN NGASA AREJEA YANGA

Winga machachali wa timu ya Mbeya City,Mrisho Khalifani Ngasa amejiunga rasmi na klabu ya Yanga kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Ngasa ni miongoni mwa wachezaji ambao wanapendwa na mashabiki wa timu ya Yanga anarejea Yanga kwa mara ya tatu ndani ya klabu hiyo baada ya awali kuhamia katika vilabu tofauti ikiwemo Azam FC,Simba,Fanya ya Oman na Free State ya nchini Afrika ya Kusini.

Taarifa zinaeleza Ngasa amesaini mkataba wa mwaka mmoja na wakati wowote kuanzia atatamburishwa rasmi ndani ya klabu hiyo.

No comments