BMT WATANGAZA UCHAGUZI WA CHANETA

Baraza la michezo la Taifa (BMT) limetangaza uchaguzi mkuu wa chama cha mchezo wa Netiboli Tanzania (CHANETA) unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 septemba mwaka huu huko mkoani Dodoma.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo,Afsa Habari wa BMT,Najaha Bakali alisema kwamba fomu za uchaguzi zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 15 agost katika ofsi za baraza la michezo la Taifa zilizopo uwanja wa Taifa.

Nafasi ambazo zinawaniwa ni pamoja na,

1.Mwenyekiti nafasi moja
2.Makamu mwenyekiti nafasi moja
3.Katibu mkuu nafasi moja
4.Katibu msaidizi nafasi moja
5.Mweka Hadhina nafasi moja
6.Wajumbe nafasi sita (6) wa kuchaguliwa.

Gharama za fomu za uchaguzi ni shilingi laki moja (100,000/=) kwa nafasi tano za juu na shilingi elfu hamsini kwa (sh.50,000/=) kwa nafasi za wajumbe.

No comments