SHIJA RICHARD AZINDUA KAMPENI

Mgombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF, Shija Richard leo hii amezundua rasmi kampeni zake kuhakikisha anawashawishi wapiga Kura wamuweke madarakani.

Akiongea mbele ya waandishi wa  habar wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo Shija alisema kwamba moja ya sera yake ni kuweka mipango ya muda mrefu ikiwemo kujenga kituo cha kukuzia vipaji cha wanamichezo kitakachojengwa mkoani Dodoma.

Katika hatua nyingine Shija Richard alisema kwamba mbali ya kuwa na mpango wa muda mrefu lakini atahakikisha anaimalisha TFF kwenye uongozi ili kusewepo kwa mwingiliano wa majukumu.

No comments