HARUNA NIYONZIMA AWASHUKURU WANA YANGA

Kiungo machachali wa timu ya Simba,Haruna Niyonzima amewashukuru mashabiki wa timu ya Yanga ambao kwa kipindi chote ambacho alikuwa kwenye timu hiyo walikuwa wanamuunga mkono.

Niyonzima alisema kwamba Yanga ni timu ambayo amedumu kwa muda mrefu kuliko timu zote alizochezea hivyo kwake kitu muhimu ni kuwashukuru kwa sapoti ambayo wamempa kwa muda wote.

Alisema kwamba hata ikitokea akafanikiwa kuwafunga Yanga katika mechi ngao ya jamii itakayopigwa agost 23 basi atashangilia kwa heshima.

No comments