YANGA WAMKATAA MRISHO NGASA

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba hawatakuwa na mchezaji Mrisho Khalifan Ngasa katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara,kwani hayupo kwenye usajili wa wachezaji ambao wameuwasilisha TFF.

Afsa Habari msaidizi wa Yanga,Godlsten Anderson Chicharito ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba Ngasa hataweza kuichezea timu hiyo kwa kuwa si miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na Yanga.

Kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili siku ya jana kumekuwa na taarifa kuwa mchezaji huyo alikuwa mbioni kujiunga na Yanga lakini jambo hilo limeshindikana kwani tayari dirisha la usajili kwa wachezaji wa ndani lishafungwa rasmi.

No comments