MWAKALEBELA AJA NA SERA YA KUJENGA KITEGA UCHUMI

Wagombea mbalimbali wanaowania nafasi za uongozi kunako shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,wameendelea kunadi sera zao kuhakikisha kuwa wanawashawishi wapiga kura wawaweke madarakani.

Fredrick Wilfred Mwakalebela leo hii amezindua rasmi kampeni zake za kuwania nafasi ya Urais wa TFF,mbele ya waandishi wa Habari na kueleza maswala mbalimbali ya uongozi wake.

Mwakalebela alisema kwamba endapo kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa TFF,moja ya mipango yake ni swala la utawala bora na kuimarisha timu zote za Taifa kwa kuandaa mpango maalumu wa miaka minne.

Aidha alisema kwamba, mkakati wake mwingine ni kujenga kitega uchumi kikubwa ambacho ni endelevu kitakachojengwa kwenye ofsi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.

No comments