TANZANIA YAPANDA KATIKA VIWANGO VYA FIFA

Tanzania imefanikiwa kupanda  katika viwango vya ubora vinavyotolewa na FIFA kwa nafasi 25 kutoka nafasi ya 139 hadi 114.

Brazil imerejea kileleni kwa kushika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Ujerumani,Argentina,Switzerland na Poland iliyoshika nafasi ya tano kwenye viwango hivyo.

Katika ukanda wa Afrika mashariki Uganda imeendelea kuongoza kwa nafasi ya kwanza pia ikiwa ya 73 kwa dunia ikifuatiwa na Kenya kwenye nafasi ya pili kwa jumla ikishika nafasi ya 82.

Misri imeshika namba moja kwa Afrika baada ya kushika nafasi ya 25 kwa dunia akifuatiwa na Congo Dr katika nafasi ya pili baada ya kukamata nafasi ya 28 katika viwango vya jumla.


No comments