MKWASA AWAPONGEZA AZAM FC

Uongozi wa klabu ya Yanga umewapongeza viongozi wa klabu ya Azam FC kwa kuweza kumuidhinisha mchezaji wao Gadiel Michael kujiunga na Yanga licha ya kuwa na mkataba wa miezi mitano.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charse Boniphace Mkwasa alisema kwamba kitendo walichofanya Azam ni cha kiungwana ambacho kinastahili kupongezwa.

Mchezaji huyo kesho anatarajiwa kuonekana katika kikosi cha Yanga kitakachoshuka dimbani kumenyana na Ruvu Shooting,mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi.

No comments