OKWI,HARUNA NIYONZIMA AMELETA CHANGAMOTO NDANI YA SIMBA

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Simba,Emmanuel Okwi amesema kwamba kiungo wa timu hiyo,Haruna Niyonzima ameleta changamoto kubwa katika kikosi cha Simba kwani ni miongoni mwa wachezaji bora wenye uwezo wa kuisadia timu.

Okwi alisema kwamba ujio wa Haruna ndani ya Simba ni swala la kuwapongeza viongozi ambao wametambua ubora na thamani ya mchezaji na anaamini kiwango chake kitaleta ushindani wa hali ya juu katika timu.

Alisema kwamba kilichopo kwa kipindi hiki ni wachezaji kuwa na ushirikiano wa kutosha ili kuleta muunganiko wa kutosha kuweza kuipa timu mafanikio ikiwemo kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi agost 26 mwaka huu.

No comments