HAMIS KILOMONI ASIMAMISHWA UWANACHAMA

Mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa klabu ya Simba Hamis Kilomoni ameondolewa kuwa mdhamini wa klabu na nafasiyake imechukuliwa na Adam Mgoi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kilosa.

Kilomoni amesimamishwa uanachama kufuatiwa maamuzi yaliyofikiwa katika mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika leo hii katika ukumbii wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Pia mkutano mkuu umemchagua Prof.Juma Kapuya kuwa mdhamini wa klabu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na marehem Kleist Sykes.

Maamuzi hayo ya kumsimamisha uwanachama Kilomoni yamefanyika baada ya kiongozi huyo wa baraza la wadhamini kwenda Mahakamani kupinga mkutano mkuu wa wanachama.

No comments