TAWI LA YANGA KIBAHA MAILI MOJA WAPANGA KUFANYA SHEREHE

Wanachama wa klabu ya Yanga,Tawila la Kibaha Maili Moja hapo kesho wanataraji kuwa na kikao kujadili maswala mbalimbali ya klabu ikwemo kuandaa sherehe ya kuipongeza timu hiyo kwa kufanikiwa kuchukua ubingwa kwa mara ya tatu mfufulizo.

Katibu msaidizi wa tawi hilo Hamis Mkumba,alisema kwamba hapo kesho wanachama wa tawi hilo watakutana kuanzia mishale ya saa 10 jioni maeneo ya Kontena bar kwa ajili ya kujadili maswala mbalimbali.

Alisema kwamba sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 13 mwezi huu ambapo kutafanyika maswala mbalimbali ikiwemo kuwaombea dua wazee wa klabu hiyo waliotangulia mbele ya haki kama ilivyo tamaduni ya klabu hiyo.

Mkumba amewataka wanachama wa tawi hilo la Kibaha Maili Moja kujitokeza kwa wingi hapo kesho kwenye kikao hicho ili kufanikisha swala hilo.

No comments