BAADA YA KUTUA SIMBA NIYONZIMA ASEMA HAYA

Baada ya kutamburishwa rasmi na uongozi wa klabu ya Simba,winga mahili wa zamani wa timu ya Yanga na APR ya nchini Rwanda,Haruna Niyonzima amesema kwamba kwa sasa hatakuwa na mambo mengi ya kuzungumza.

Niyonzima alisema kwamba kwa sasa yeye ni mchezaji halali wa timu ya Simba hivyo vitendo vyake vitaonekana uwanjani.

Niyonzima aliyejiunga na Simba akitokea Yanga ni miongoni mwa wachezaji ambao usajili wake umekuwa gumzo kwa muda mrefu,hii inatokana na kiwango bora alichokionesha akiwa na Yanga kwa misimu sita.


No comments