"BYE BYE YA MOTO BAND"

Na DJ Rodger,Dar es salaam
OfCoz Bila Shaka Unakumbuka Vizuri Ujio Aslay  Enzi hizo Akiitwa Dogo Aslay Wakati Akitoka Na Ngoma ya yake Kwanza Kabisa ya"Naenda Kusema Kwa Mama"Moja Kati ya hit Song Na Kazi Makini kabisa,kazi Ambayo ilimfanya Watanzania Wengi Wamtambue Na Hasa Watoto Wadogo Sababu Ujumbe wake Ulikaa Kitoto Zaidi.

Baada ya Hapo Aslay Kufanya Vizuri na Rekodi zake Kadhaa Aslay Alijiuunga na Bandi ya Mziki wa Kizazi Kipya Akiitwa Ya Moto Band Iliyookuwa Ikiimilikiwa Na Said Fella aka Mkubwa Fella Moja Kati Mameneger Wakubwa sana hapa Nchini Tanzania.

Kabla hapo Said Fella Aliwahi Kumiliki Kundi la Mziki wa Bongo flevar Kundi la Wanaume TMK lilokuwa Likuundwa na Juma Nature,Chegge,Temba,KR Mulla,Dolo na Wengine Wengi  "Wazee wa Mapanga Shaa!! Shaa!!" Moja ya Vibwagizo vya Kundi hilo,Lakini Mwisho wa Siku Kundi hilo nalo Lilisambaratika Chanzo Chake Ambacho Mpaka Leo Hakijulikani Ambapo Kila Moja Akiuulizwa Humtupia Mpira Mwenzake.

Wakiwa Vijana Wenye Umri Mdogo kabisa Lakini Mambo yao Yalikuwa Ni Makubwa Kupita kiasi Kutokana na Umahiri wa Kutumbuiza Jukwaani,YaMoto Bandi Ilifanya Vizuri  Nakupendwa na Kila Rika Hata Wakati Mwingine Kufikia Kufanya Matamasha Makubwa Ndani Na Nje ya Nchi Na Ilipewa Heshima Kubwa Sana hata Kuaalikwa Kutumbuiza Kwenye Shughuli Kubwa za Kitaifa Kama Shughuli za Kisiasa Nk.

Story Ambazo Zinatrend Hivi Sasa Ni Kuhusu Bandi hiyo Kuwa Imesambaratika Baada Ya Aslay Kuanza tena  Kufanya Kazi zake Kama Solo Artist
Na Je Ni Kweli Ya Moto Bandi Nayo Ndio Bye Bye!! Kama Ilivyokufa Wanauume TMK?? Maana  Tumeoona Baadh ya Wasanii wa YaMoto Band Kama Aslay Akiuulizwa Kwenye Interview za Radio Station Hapa Bongo  Hudai Kuwa Band  hiyo bado Ipo Lakini Ukichunguza Kiuundani YaMoto Itakuwa Imesambaratika Na Haitakuwepo.

Hata Ukikumbuka Vizuri Makundi ya Zamani Kama Daz Nundaz,HBC,Gangwe Mob Nk Nao walikuwa Wakiuulizwa Walikuwa Wakisema Kundi Bado Lipo Lakini Mpaka Sasa Makundi hayo hayapo na Baadhi yao Wameshuka Kimuzki.

Lakin Kwa Wao Baada ya Aslay Tumeeona Msanii Kama  Beka Flavour Aliyekuwa Ndani ya Bandi hiyo Naye Kafanya Project yake binafsi Ngoma yake Kwanza Ikiitwa  Libebe,Vivyo hivyo Pia Kwa Enock Bella Naye Anaproject Mpya Kafanya Pale Maxmizer

Naaaaa Vipi kuhusu Upande wa Maromboso na yeye???Maromboso Mpaka Sasa hajaachia Project Yake Binafsi,Story Ambazo Zipo Ni Kuwa Kachukuliwa Na WCB Recoding Lebol Ambayo Inayofanya vizuri sana Ndani na Nje ya Nchi Chini ya Diamond Platnums.

No comments