YANGA WAFIKIA MAKUBALIANO NA TAIFA JANG'OMBE

Uongozi wa timu ya Taifa Jang'ombe ya visiwani Zanzibar umesema kwamba wameshakubaliana na klabu ya Yanga juu ya mauzo ya mchezaji wao Abdalah Haji Shaibu maarufu maarufu kwa jina la" Ninja"

Katibu wa timu hiyo Mohd Maulid alisema kwamba uongozi wa klabu ya Yanga umeahidi kuwapatia fedha za usajili siku ya jumatano ya wiki inayoanza hapo kesho.

"Mashabiki wa Taifa Jang'ombe wanapaswa kufahamu kuwa sisi viongozi tushakubaliana kila kitu na Yanga kuhusu mauzo ya mchezaji na kwa sasa kilichosalia ni kutupatia fedha tu ambapo kwa mujibu wao wameahidi kutupatia siku ya jumatano"alisema Maulid.

No comments