TAIFA JANG'OMBE WAPANGA KUIGOMEA YANGA

Uongozi wa timu ya Taifa Jang'ombe ya visiwani Zanzibar,umesema kwamba hawatakuwa tayari kumuachia mchezaji wao Abdalah Haji Shaibu maarufu kwa jina la "Ninja"kuichezea Yanga endapo klabu hiyo itashindwa kuwalipa fedha zao za usajili wa mchezaji huyo.

Katibu mkuu wa Taifa Jang'ombe,Mohd Maulid amesema kwamba licha ya kukubaliana na klabu hiyo kwenye maswala ya kimaslahi lakini hadi leo hii Yanga bado hawajawalipa fedha zao.

Alisema kwamba Yanga awali waliwapa taarifa kwamba wangewalipa fedha hizo kwa siku ya jana lakini jambo hilo halikufanyika hadi leo hii.

Alisema kwamba kwa sasa hawatawapigia tena simu hadi hapo watakapoamua wenyewe,kwa kuwa hawana shaka na swala hilo,hivyo watakachofanya ni kutotoa ITC ya mchezaji ligi itakapoanza.

No comments