SIMBA YAKAMILISHA USAJILI WA SALIM MBONDE

Simba imedhamiria kufanya kweli msimu ujao hasa kwenye uboreshaji wa kikosi chao hii inatokana na leo hii kukamilisha usajili wa mchezaji Salim Mbonde ambae awali alikuwa mchezaji tegemeo wa wakata miwa wa Manungu Turiani mkoani Morogoro Mtibwa Sugar.

Licha ya viongozi wakuu wa Simba,Rais na Makamu wake kuwa rumande lakini viongozi waliosalia bado wanaendeleza na mapambano ya usajili kwa lengo la kukiboresha kikosi chao ambacho msimu ujao kitashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mbonde ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri kwenye michuano ya COSAFA na kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu waliokuwa na mchango mkubwa katika timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ambayo imeshika nafasi ya tatu.

No comments