GOR MAHIA WATUA DAR KUIVAA EVERTON

Timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya tayari imeshawasili hapa nchini kwa ajili ya kujiandaa na pambano la kimataifa la kirafiki dhidi ya timu ya Everton ya nchini England.

Gor Mahia siku ya alhamisi itashuka uwanjani kumenyana na Everton, mechi inayotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Everton kwa upande wao wanataraji kuwasili hapa nchini siku ya kesho kwa ajili ya mchezo huo ambao umeratibiwa na kampuni inayojiusisha na maswala ya ubashiri ya SportPesa.

Gor Mahia imepata nafasi hiyo ya kucheza na Everton baada ya kufanikiwa kuwa mabingwa wa michuano ya SportPesa iliyofanyika hapa nchini.

No comments