WAZIRI WA RWANDA AMPA USHAURI HARUNA NIYONZIMA
Na Said Ally Mwandike,Mwanza
Waziri wa Michezo na Utamaduni nchini Rwanda,Habyarimana Florent amemtaka mchezaji Haruna Niyonzima kwenda kucheza kwa kiwango kikubwa kama alivyokuwa anaitumikia klabu ya Yanga huko anapotaraji kusaini mkataba mpya.
Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPOT,Florent alisema kwamba Niyonzima ni moja ya wachezaji wazuri na wenye sifa kubwa kwa nchi hivyo ni vyema huko anapokwenda iwe Simba au klabu nyingine basi anatakiwa kucheza kwa juhudi kubwa.
"Kule Yanga amecheza vizuri na nafikili kwamba akifika kule Simba acheze vizuri,kwa sababu kazi yake ni kucheza ndio anaishi maisha yake, ikiwa akifika kule akicheza vibaya hatapata chochote na akifiki kule Simba afanye vizuri kama tunavymjua ili awafurahishe mashabiki wa Simba"alisema Florent.
Aidha alisema kwamba mashabiki wa soka hususani wa klabu ya Yanga wanapaswa kufahamu kuwa mchezaji kazi yake ni mpira,hivyo kuondoka kwa Niyonzima ni moja ya malengo yake ya kusaka fedha ambazo zitaweza kumsaidia katika mipango yake ya maisha.
Hata hivyo hadi kufikia sasa bado hakuna taarifa rasmi juu ya usajili wa Haruna Niyonzima lakini taarifa za awali zinaeleza kuwa msimu mjao huenda akaonekana ndani ya klabu ya Simba baada ya kufikia makubaliano ya usajili.

Post a Comment