KOCHA MBAO FC AIKANA SIMBA SC

Na Said Ally Mwandike,Mwanza
Kocha mkuu wa timu ya Mbao FC ya Ilemela mkoani Mwanza Ettiene Ndayiragije amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuzipuuzia taarifa zinazoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa yuko mbioni kuikacha timu hiyo na kujiunga na klabu ya Simba.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPOT,Ndayiragije amesema kwamba hawezi kuvizuia vyombo vya habari kuandika taarifa wanazozitaka lakini swala la yeye kujiunga na klabu ya Simba hawezi kulizungumzia kwa wakati huu kwasababu bado yupo katika klabu ya Mbao FC.

Alisema kwamba kwa sasa nguvu zake amezielekeza kwenye klabu yake ya Mbao FC ili kukijenga kikosi cha timu hiyo kiwe bora na kiendeleze upinzani wa hali ya juu katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kuanza mwezi ujao.

Hata hivyo amesema kwmba kwa sasa bado anaendelea na mchakato wa kusaka wachezaji kupitia programu maalumu kabla ya kuwapa mikataba kwa wachezaji watakaonekana wanafaa kuitumikia timu hiyo.

No comments