SIMBA WAJIBU KAULI YA ABDI BANDA

*Simba Sports Club* 
*D'salaam, Tanzania*
*11-7-2017.* 
    *TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
*____________________________________________*
Klabu ya Simba inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na malalamiko ya mchezaji Abdi Banda ambae alilalalamika jana kupitia vyombo vya habari,kuwa klabu imemkatalia kumpa barua ya kumuacha *(REALISE LETTER)* ilhali yeye amepata Timu huko Afrika kusini na huku akiwa amemaliza mkataba wake.

Ni kweli Banda amemaliza Mkataba na klabu, na jana alikuja ofisini kwetu kutaka barua hiyo, lakini akakumbushwa kuwa,ukiwa umemaliza Mkataba haupaswi kupewa barua hiyo,wanaoandikiwa barua hiyo ni waajiriwa ambao bado wana mikataba na labda kwa sababu yoyote ile,klabu inaamua kuachana nao.

Lakini kwa kuwa Banda aliitaka hyo barua, akaambiwe aandike barua fupi tu ya kuomba Realise Letter, ili ibaki kumbukumbu kwa klabu, lakini kwa mshangao wa maafisa wa klabu aligoma kuiandikia barua klabu na kuamua kukimbilia kwenye vyombo vya habari na Blogs.

Klabu imesikitishwa sana na kitendo hicho kinachojirudia cha kutafuta huruma kupitia Media,huku akijua kuwa anaikosea heshima klabu na kuipaka matope bila sababu.

Simba inaamini sana utamaduni wake wa miaka mingi wa kuwaruhusu wachezaji wake kwenda nje ya nchi kucheza soka, pindi wapatapo nafasi hiyo,lakini inasisitiza sana suala la utaratibu,haijawahi kutokea kokote duniani,mchezaji aliyemaliza mkataba kudai Realise letter,na kiukweli tumeshangazwa pia na baadhi ya vyombo vya habari kulishupalia jambo hili bila hata kutusikiliza (kubalance story).

Na kwa kupitia barua hii, klabu inawaambia haitafanya kazi kwa shinikizo la mtu au chombo chochote kile huku tukifahamu ni kinyume na utaratibu na utamaduni wa mchezo huu unaopendwa duniani kote.

*Mwisho*
tunawaambia kwa sasa tutakuwa na udhibiti mkubwa wa wachezaji wetu na benchi la ufundi kuongea na vyombo vya habari na blogs, huku pia ikimsisitiza Banda akitaka barua yetu ni wajibu wake kuandika barua pia,vnginevyo klabu yetu inamtakia mafanikio makubwa huko aendako.
IMETOLEWA NA
IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO
SIMBA SC.
*SIMBA NGUVU MOJA*

No comments