MINZIRO AJIONDOA MWENYEWE SINGIDA UNITED

Uongozi wa timu ya Singida United umesema kwamba kocha wao msaidizi Fred Felix Minziro amejiondoa mwenyewe katika timu hiyo baada ya yeye mwenyewe kuamua kukaa pembeni katika timu hiyo.

Katibu mkuu wa Singida United,Abdulrahman Sima amesema kwamba watanzania wanapaswa kufahamu jambo hilo na wala sio kusema kuwa klabu ndio imeachana na Minziro.

Sima alisema kwamba amekuwa akimpigia simu Minziro kwa ajili ya kutaka kufahamu mustakabali wake lakini kocha huyo ameshindwa kupokea simu yake.

Alisema kwamba pia amesikia taarifa kuwa Minziro amejiunga na klabu ya KMC inayoshiriki ligi daraja la kwanza kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.


Hata hivyo Sima ameendelea kusema kwamba kwa upande wao nafasi ya Minziro bado ipo ambapo kama mwenyewe ataamua kurejea katika timu uongozi utampokea kwa Baraka zote.

No comments