NIZAR KHALIFAN AIPA NAFASI SINGIDA UNITED

Nahodha wa timu ya Singida United,Nizar Khalifani amesema kwamba kwa sasa kikosi cha timu hiyo kinajiandaa vyema kwa ajili ya ushiriki wao wa ligi kuu ya Tanzania bara inayotaraji kuanza agost 26 mwaka huu.

Nizar ameyasema hayo leo hii akiwa uwanja wa Nyamagana uliopo mkoani Mwanza walipoweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao baada ya uwanja wao wa Namfua kuwepo kwenye ukarabati.

Alisema kwamba mipango yao ni kuona wanafanya vizuri katika michezo yao ya ligi ikwemo mechi yao ya kwanza dhidi ya Mwadui wanayotaraji kucheza wakiwa ugenini mkoani Shinyanga.

Hata hivyo alisema kwamba kutokana na maandalizi ambayo wanayoyafanya anaamini licha ya kuwa ugeni katika ligi anaamini Singida United itafanya vizuri na kuwashangaz watanzania.

No comments