TIMU SHIRIKI LIGI YA ZANZIBAR MSIMU UJAO ZAJULIKANA

Na,Sleiman Ussi,Zanzibar
Msimu mpya wa mwaka 2017-2018 kutakuwa na ligi one na ligi two ambapo ligi one ndio ya juu kabisa yani Primier ligi na ligi two itakuwa daraja jipya kwa Zanzibar.

Ligi hizo zote zitatoa wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano ya Kimataifa, ambapo Ligi one itatoa muwakilishi wa Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika wakati ligi two itatoa muwakilishi wa Kombe la Shirikisho Barani humo.

Timu hizo 12 zilizofanikiwa kucheza ligi kuu (Ligi 1) msimu mpya wa mwaka 2017-2018 ni JKU, Jang’ombe Boys, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe, Polisi, KMKM kwa upande wa Unguja na Pemba ni Jamhuri, Kizimbani, Mwenge, Okapi, Chipukizi na New Stars.

Kwa upande wa timu 16 zitakazocheza ligi 2 msimu mpya wa mwaka 2017-2018 kati ya hizo 8 za Unguja na 8 za Pemba ambapo za Unguja ni Mafunzo, KVZ, Black Sailors, Chuoni, Kilimani City, Kipanga, Miembeni City na Charawe wakati za Pemba ni Dogomoro, Wawi Star, Shaba, Young Islander, FSC, Hardrock, Chuo Basra na Opek.

Timu 4 za mwisho za ligi 1 zitashuka daraja ligi 2, na timu 4 za juu za ligi 2 zitapanda daraja la ligi 1.

No comments