JULIO AIJIA JUU KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF

Baada ya kuenguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF kwa kigezo cha kushindwa kuwasilisha cheti za kumaliza elimu ya sekondari,Jamhuri Kiwelu Julio amesema kwamba kamati ya uchaguzi haikutenda haki kuamua kumuondoa kwenye zoezi hilo.

Julio alisema kwamba anashangaa kuona kamati ya uchaguzi inashindwa kwenda kwenye baraza la mitihani ili kujiridhisha zaidi baada ya yeye kuwasilisha maelezo yake katika kamati hiyo.

"Cheti changu mimi kilipotea sio jana wala juzi kilipotea siku nyingi hata katika uchguzi wa Simba niliambiwa nipeleke barua ya Polisi kuonyesha cheti changu kuwa kilipotea,hatua ya pili niende kwenye gazeti la serikali nifanye hivyo na kweli nimefanya hivyo wao kama kamati ya uchaguzi walienda NECTA wakapata jibu na nilipitishwa kugombea baada ya kujiridhisha kuwa nina cheti sasa naishangaa hii kamati ya TFF"alisema Julio.

Alisema kwamba kwa sasa yeye bado hajawa na mtazamo kamili wa kukata rufaa au la, kwani anaweza akaachana na swala hilo au akaendelea lakini bado ana hofu huenda akakata rufaa na pia asipite kwenye uchaguzi hivyo akapoteza fedha za bure.

No comments