MAYANGA ASEMA STARS IKO TAYARI KUWAVAA RWANDA

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,Salum Mayanga amesema kwamba kikosi chake kipo tayari kwa mechi ya kesho dhidi ya Rwanda katika mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza kwa fainali za Afrika,mchezo unaotarajiwa kuchezwa mkoani Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Mayanga ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba wachezaji wote wako vizuri na kila mmoja ana hamasa ya kufanya vizuri kwenye pambano hilo ambalo linataraji kuwa na ushindani wa hali juu kutoka kwa pande zote.

Wapinzani wao timu ya Rwanda tayari imeshawasili jijini Mwanza kwa msafa wa makundi mawili ambapo kundi la kwanza la wachezaji liliwasili mapema asubuhi ya leo hii tayari kwa pambano hilo.

No comments