ISRAEL NKONGO KUCHEZESHA PAMBANO LA EVERTON

Mwamuzi Israel Nkongo ndie atakaechezesha pambano la kimataifa la kirafiki kati ya timu ya Everton ya nchini England dhidi ya Gor Mahia ya nchini Kenya.

Nkongo atasaidiwa na Ferdinand Chacha pamoja na Frank Komba ambao hawa watashika vibendera huku mwamuzi wa akiba akiwa Elly Sasii na Michael Wambura atakuwa kamishina wa pambano hilo linalotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Everton wanataraji kuwasili hapa nchini siku ya kesho huku Gor Mahia wao wakitaraji kuwasili leo hii ambapo kwa mujibu wa waratibu wa pambano hilo kampuni ya SportPesa wamesema kwamba maandalizi kwa ujumla yamekamilika.

Kiingilio cha chini kwenye pambano hilo ni shilingi elfu tatu huku kiingilio cha juu ni shilingi elfu nane ambapo tiketi hizo zinauzwa kwa utaratibu uleule wa njia ya mtandao kupitia kampuni ya Selcom.

Pambano hilo linataraji kuwa na hamasa kubwa hasa wadau wa soka wakiwa na shauku ya kutaka kumuona mchezaji Wayne Rooney aliyesajiliwa na klabu hiyo ya Everton ambae kwa mujibu wa waratibu wa kampuni hiyo wamedai kuwa huenda Rooney akawemo kwenye kikosi hicho kinachowasili hapo kesho.

No comments