WAZEE WA SIMBA WATAKA WAJUMBE WAO WAFUNGIWE

Na Anaseli Stanley,Dar es salaam
Wazee wa klabu ya Simba wameitaka serikali kupitia kwa msajili wa vyama vya michezo na vilabu kuwafungia wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ya Simba kutokana na viongozi hao kutotoa taarifa ya mapato na matumizi tangu waingie madarakani mwaka 2014.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii mratibu wa wazee wa Simba,Felix Makua amesema kwamba wazee wa klabu hiyo wanashangazwa na jambo hilo, hivyo ndio maana wameamua kuchukua hatua ya kuiomba serikali ili iwasaidie swala hilo ikwemo kuwafungia wajumbe hao.

Hii si mara ya kwanza kwa wazee hao kutoa matamko mbalimbali kwa uongozi uliopo madarakani wakiamini kwamba kuna mambo mengine yanafanywa na uongozi kinyume na taratibu za klabu ya Simba.

No comments