SIMBA WAMTUPIA VIRAGO JOSEPH OMOG

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza rasmi kuachana na kocha mkuu wa timu hiyo Joseph Omog baada ya kwa pande mbili kukubaliana kuvunja mkataba kwa makubaliano maalum.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari imeeleza kuwa kwa kipindi hiki timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na pia itaendelea na mazoezi hapo kesho kabla ya kupumzika siku ya jumatatu kwa mapumziko ya Christmas kabla ya kurejea siku ya jumanne kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi.

Katika hatua nyingine klabu hiyo imewaomba radhi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa FA ambapo wekundu hao wa Msimbazi waliondoshwa katika michuano hiyo baada ya kufungwa na timu ya Green Worriers kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-4.


No comments