JKT RUVU KUTUMIA MCHEZO WA FA KUENDELEZA KUMBUKUMBU NA HESHIMA KWA ASKARI WA JWTZ
Na Said Ally
Kikosi cha timu ya JKT Ruvu hapo kesho kinataraji kushuka dimbani kumenyana na timu ya Mvuvumwa FC katika mchezo wa kombe la FA unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia saa moja usiku.
Afisa Habari wa timu ya JKT Ruvu,Costantine Masanja alisema kwamba kikosi cha timu hiyo ambacho kinaongozwa na kocha Bakari Shime kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao anaamini utakuwa na ushindani wa hali juu.
Alisema kwamba timu ya JKT Ruvu katika mchezo huo itafunga vitambaa vyeusi na kusimama kwa dakika moja kabla ya mchezo ikiwa ni kumbukumbu na heshima kwa askari wa JWTZ 14 waliokufa nchini Congo katika jukumu la ulinzi wa Amani chini ya umoja wa mataifa.

Post a Comment