MANENO YA CRISS WAMARYA BAADA YA KUACHIA NGOMA YAKE MPYA

Na Said Ally
Mkali wa bongo Frever hapa nchini,Criss Wamarya ametamba kuendelea kufanya vizuri kwenye soko la sanaa ya muziki kupitia nyimbo zake mbalimbali ambazo zinatamba katika runinga,radio na sehemu mbalimbali.

Wamarya ambae si mgeni kwa wadau wa muziki wa bongo Frever kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya inayojulikana kwa jina la "Kolo"uliotengenezwa na Produce Zest ambao unapatikana sehemu mbali kuanzia sasa kupitia mitandao ya kijamii.

Alisema kwamba dhamira yake ni kuona anaitangaza vyema nchi sehemu mbalimbali kupitia kazi yake ya sanaa hasa kutokana na kipaji alichobalikiwa cha uimbaji.

Miongoni mwa ngoma ambazo zimemtamburisha Wamarya ni pamoja na wimbo wake wa kilomita sita ambao ulipokelewa vizuri na wadau wa muziki kabla ya kuachia ngoma kibao tokea hapo ikiwemo Sina,Cheusi Mangara na nyinginezo.

No comments