SIMBA WAAMUA KUWA WANYONGE KWA LIPULI FC

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Simba umewasilisha rasmi barua katika uongozi wa Lipuli FC,ukihitaji kufanya majadiliano ya kumaliza swala la mchezaji Asante Kwasi anaedaiwa kusajiliwa na klabu hiyo ya wakendu wa Msimbazi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika uongozi wa klabu ya Lipuli FC,inaeleza kuwa klabu hiyo imekili kupokea barua hiyo na wao wameridhia kuwakaribisha Simba kufanya majadiliano juu ya usajili wa mchezaji  Asante Kwasi.

Simba imeamua kuchukua jukumu hilo baada ya kubaini kuwa Kwasi bado angali na mkataba na Wanapaluhengo hao wa mkoani Iringa hivyo kwao wamedhamiria kufanya majadiliano na Lipuli na endapo kama wataridhiana basi mchezaji huyo atakuwa ni miongoni mwa wachezaji wa Simba.

Hata hivyo uongozi wa Simba kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo Hans Pope umesema kwamba katika dirisha dogo la usajili Simba imeachana na mchezaji mmoja tu ambae ni Method Mwanjali lakini wengine wote walio salia mbali na Jamali Mnyate aliyepelekwa kwa mkopo katika klabu ya Lipuli FC wataendelea kuwepo ndani ya klabu hiyo.

No comments