HILI NDILO DAU WALILOPEWA LIPULI FC BAADA YA MAUZO YA ASANTE KWASI


Na,Said Ally
Uongozi wa klabu ya Lipuli FC,umesema kwamba umeridhia mchezaji wao Asante Kwasi ajiunge na klabu ya Simba baada ya kupata muafaka katika majadiliano yao.

Mwenyekiti wa timu ya Lipuli FC,Ramadhani Mahano ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba klabu ya Simba imekubali kulipa kiasi cha shilingi milioni 25 ili mchezaji huyo aweze kuitumikia Simba kwa kipindi kilichosalia katika mkataba wake wa mwaka mmoja.

Mahano alisema kwamba kiwango hicho cha shilingi milioni 25 ndicho kilichohitajika na uongozi wa Lipuli kutokana na mkataba wake uliosalia wa mwaka mmoja.

Alisema kwamba fedha hizo zote tayari zimeshaingizwa kwenye akaunti ya timu hivyo kwa upande wao kama uongozi tayari umeshawaandikia barua Simba ya kuwaruhusu kumtumia mchezaji Asante Kwasi.

Hata hivyo Mahano amewataka mashabiki wa Lipuli FC,kutokua na wasiwasi wowote juu ya kuondoka kwa mchezaji huyo kwani ana imani wachezaji waliosalia wataziba pengo lake na timu itaendelea kufanya vizuri.

No comments