YANGA YATEUA KAMATI YA MABADILIKO YA UENDESHAJI WA TIMU

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga leo hii umetangaza kamati ya mabadiliko ambayo itakuwa na jukumu la kuratibu maswala mbalimbali ya mfumo mpya wa uendeshaji wa timu.

Kamati hiyo ya mabadiliko iliyotangazwa na kaimu mwenyekiti Clement Sanga mbele ya waandishi wa Habari ina jumla ya watu sita.

1.Alex Mgongolwa-M/kiti ambae ni mwanasheria
2.Prof Mgongo Fimbo-mtaalam wa katiba sheria za ardhi
3.Meki Sadiki-Mkuu wa mkoa mstaafu
4.Mohamed Nyenge-mchumi na mwenyekiti wa kamati ya uchumi na fedha
5.George Fumbuka-mshauri masuala ya uwekezaji
6.Felix Mlaki-mchumi na mtaalam wa masuala ya fedha.

No comments