BAADA YA KIPIGO MANARA ATOA KAULI NZITO

Na,Kilian France
Baada ya kushindwa kutinga katika hatua ya 32 bora ya michuano ya kombe la Azam Sports Federation,mkuu wa idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba,Haji Manara ameonyesha kusikitishwa na kitendo hicho kwa timu kubwa kama Simba kufungwa na timu ya daraja la pili ya Green Worriors.

Kupitia ukurasa wake wa instagram,Manara aliandika ujumbe unaonyeshwa kuhudhunishwa na kipigo hicho cha kufungwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3 baada ya dakika 90 timu hizo kufungana bao 1-1,goli la Hussein Bunu kwa kichwa na John Boko kwa mkwaju wa penati.

"Shame..Aibu..fedheha..Aivumiliki..Tumewakera fans wetu zaidi ya twenty milions..nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba...Aibu ya mwaka"aliandika Manara kupitia ukurasa wake wa instagram huku akiweka alama ya mshangao.

Katika mchezo wa jana uliochezwa kwenye uwanja Azam Complex ulioko Chamazi mlinda mlango Aishi Manura alifanikiwa kupangua penati moja iliyopigwa na Zuakuu Mgala kabla ya George Ossey kupiga nje.

Kiungo Jonasi Mkude,Mohamed Hussein na Muzamiru Yassin walikosa penati kwa upande wa Simba na kupelekea wekundu hao wa Msimbazi kuvuliwa ubingwa wa michuano hiyo ya kombe la FA ambapo bingwa wa michuano hiyo ndie anaeiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Hata hivyo katika mchezo huo Green Worriors walipata pigo dakika za mwisho mwisho baada ya mchezaji wao Adam Said kuzawadiwa kadi nyekundu na mwamuzi Israel Nkongo.

No comments